Jumanne 22 Julai 2025 - 04:05
Maandamano ya kupinga Uzayuni yameendelea nchini Jordan

Hawza/ Mitaa ya maeneo kadhaa ya Jordan tangia jana imeshuhudia maandamano ya wananchi dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Ghaza, wananchi wa Jordan, licha ya hatua kali za kiusalama zilizowekwa na serikali, hawawezi kuwasahau majirani zao wanyonge; hivyo basi, kwa kupaza kauli mbiu za kuwatetea watu wa Ghaza, wamejitokeza mitaani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika miezi ya hivi karibuni, licha ya upinzani wa serikali ya Jordan dhidi ya maandamano yanayofanywa na wananchi dhidi ya utawala wa Kizayuni na kwa ajili ya kuwatetea watu wa Ghaza, mji mkuu wa Jordan umekuwa ukishuhudia maandamano ya kupinga hali hiyo.

Ukaribu wa kiutamaduni na kijiografia kati ya watu wa Jordan na watu wa Palestina umesababisha tangu mwanzoni mwa vita vya Israel dhidi ya Ghaza, pamoja na marufuku ya maandamano kutoka kwa serikali na vyombo vya usalama, wananchi wameonesha ghadhabu na kutoridhika kwao kwa kupaza sauti dhidi ya Israel.

Hivi karibuni, vikosi vya usalama vya Jordan vilizuia mamia ya waandamanaji wenye hasira kali kufika karibu na ubalozi wa utawala wa Kizayuni ulioko mjini Amman, mji mkuu wa Jordan. Washiriki wa maandamano hayo walitaka kufungwa kwa ubalozi wa Israel nchini Jordan na walilaani kuendelea kwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha